⚡ HABARI MPYA

NEVILLE MEENA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA RUJAT

• Maoni 0

Na Michael Abel, Dodoma.

Neville Meena amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la Waandishi wa Habari za Vijijini Tanzania (RUJAT), baada ya kuwashinda wagombea wenzake wawili, Rashid Abdullah Mtagaluka na Andrea Ashery Ngolola, kwa kupata kura 74 kati ya kura 77 zilizopigwa.

Matokeo hayo yalitangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Felix Mwakyembe, kufuatia uchaguzi wa viongozi wa RUJAT uliofanyika Oktoba 31, 2026, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Meena, ambaye amewahi kuwa Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na ni miongoni mwa waasisi wa RUJAT, alisema kura nyingi alizopewa na wanachama ni dhamana anayopaswa kuilipa kwa kuwatumikia kwa moyo wote. Aliahidi kusimamia malengo ya jukwaa hilo, ikiwemo kuhakikisha habari zinazohusu wananchi wa vijijini zinapewa kipaumbele katika vyombo vya habari.

Alisema miongoni mwa vipaumbele vyake ni kuhakikisha RUJAT inapiga hatua katika kutekeleza majukumu yake, kwa kushirikiana na viongozi wenzake kuimarisha uwezo wa waandishi wa habari katika kuandaa na kuandika habari zinazogusa maslahi ya umma, hususan yale yanayohusu maisha na maendeleo ya wananchi wa vijijini.

Katika uchaguzi huo, wanachama wa RUJAT pia walimchagua Hamida Ramadhan kutoka Mkoa wa Dodoma kuwa Makamu Mwenyekiti. Aidha, Prosper Laurent Kwigize kutoka Kasulu, Mkoa wa Kigoma, alichaguliwa tena kuwa Katibu wa jukwaa hilo kwa kupata kura 76 kati ya kura 77 zilizopigwa, huku Zena Mohamed Chitwanga akichaguliwa kuwa Mweka Hazina.

Vilevile, wanachama walichagua wajumbe saba wa Kamati Tendaji ambao ni Musa Juma Siwayombe, Devotha Martine Paul, Malunde Kadama, Rashid Abdullah Mtagaluka, Anna Robi, Andrea Ashery Ngolola na Fadhili Abdallah Mwangamola. Kwa mujibu wa marekebisho ya Katiba yaliyopitishwa na wanachama wa RUJAT, uongozi mpya wa Meena na wenzake utahudumu kwa kipindi cha miaka minne kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha waandishi wa Habari vijijini (RUJAT), wamemchagua tena Mwanahabari nguli Neville Charles Meena kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi Felix Mwakyembe akitangaza matokeo

Mwenyekiti wa RUJAT Neville Charles Meena akizungumza baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine kukiongoza chama hicho

Bw. Prosper Laurent Kwigize, Katibu wa RUJAT

Facebook WhatsApp X Barua pepe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

↑